Pages

Sunday, July 29, 2012

Internet Training for mainland Journalists in Tanzania.

Hivi karibuni mmiliki wa Blog hii alikuwa katika mkoa wa Mbeya akiendesha mada inayohusu uandishi wa habari katika enzi ya intaneti. Mafunzo yalilenga kuwa fundisha waandishi wa mikoani namna ya kutumia mtandao kama chanzo cha habari na pia kama chombo cha habari.

Kuanzia leo nitakuwa naandika kile alichokisema kila mmoja baada ya mafunzo hayo hasa kwa kuzingatia matarajio yake na maoni juu ya mafunzo.

Kwa leo naanza na mwanahabari anayefahamika kwa jina la Johnson Jabir anayefanya kazi katika redio iitwayo Mbeya FM.

Na haya ndiyo aliyoyasema:


Jina: Johnson Jabir
Kutoka: Redio Mbeya FM
Nafasi: Mwana habari

SEMINA YA SIKU 3 KUHUSU MATUMIZI YA INTANETI KATIKATASNIA YA HABARI
 
Matarajio.

Unaposemamatarajio ni nini unategemea kupata ama kufanya kutoka upande Fulani ama chanzoFulani. Kwa upande wangu nalitegemea kuona kwamba sasa ufahamu wanguutafunguliwa katika masuala mbalimbali ya matumizi ya Intaneti hasa ukizingatiakwamba katika Ulimwengu wa Utandawazi kuna umuhimu mkubwa wa mimi kamamwanahabari kujua.
 
Painilitegemea kuona napokea changamoto za intaneti nje ya mkoa wa Mbeya, Tanzaniana nje ya Tanzania. Na vipi naweza kuzikabili changamoto hizo.

Aidhanilitarajia kuwa ningepata uzoefu wa walio katika kiwango cha  juu katika matumizi ya Kompyuta katika tasnia ya habari wakionyesha uzoefu.

Umuhimu.

Umuhimu wamafunzo haya nimeupata kwani mambao mengi nimefunguliwa sana ikiwemo suala zimala Intaneti kubadili jamii ya sasa, Utafiti kupitia intaneti mabapo zamaninilikuwa sifahanyi sana pia ujuzi wa kutumia barua pepe na changamoto zakelakini kubwa zaidi ilikuwa ni Usalama wa Teknolojia ya habari.

Umuhimu huounakuja kutokana na kwamba tunakoelekea katika tasnia ya habari kunahitajikujali muda, umakini katika kazi, uharaka wa kazi yenyewe, uhakiki wa kaziyenyewe na Biashara

Ushauri.

Semina hii imeletea changamoto kubwa sana kwa tasnia ya habari mkoaniMbeya hasa ukizingatia wengi kuna baadhi ya mambo tulikuwa tukifanya tu. Shukraniziwaendee waandaji wa mafunzo haya. Ushauri ni kwamba Semina hizi zifanyike kwamwaka mara mbili tu itasaidia. Kubwa zaidi ziwalengee waandishi wa habari marabaada ya kufanya utafiti wa mwandishi huyo wa habari sio kwasababu anafahamikatu bali hata anapokuwa katika chombo chake kwani kuna wengi ni waandishi wahabari wa “kimagumashi” hiyo imeshuhudiwa katika semina hii waliotarajiwa kujawengi hawakuja. Mbaya sana hii.

Mengineyo
 
KUNAchangamoto kubwa sana katika suala zima la KLABU za waandishi habari hivyokuzileta semina hizi na kutaka klabu zisimamie ni makosa makubwa sana lakininiwashukuru tena kwamba mlifanya jambo la maana kwani mimi sikio katika PressClub lakini ni wamndishi habari ambaye nimepata mafunzo hayo hii inadhihirishanamna ambavyo mmeona changamoto ndani ya PRESS CLUB nchini Tanzania muendeleehivyo hivyo kujikita katika waandishi habari wenye nia kweli ya kufanya kazikatika tasnia hii sio kwasababu ya posho za siku za semina kwani kumekuwa nanjaa kali sana kwa wengi wa watu kutaka kila semina aendee sio kwasababu yaumuhimu  wa ile semina   baliPOSHO.

MWISHO.

No comments:

Post a Comment